nao watakusanywa pamoja kama vile wakusanywavyo wafungwa katika shimo nao watafungwa katika gereza; na baada ya muda wa siku nyingi wataadhibiwa.
Danieli 8:26 - Swahili Revised Union Version Na maono ya hizo nyakati za jioni na asubuhi yaliyosemwa ni kweli; lakini wewe yafunike maono hayo; maana ni ya wakati ujao baada ya siku nyingi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maono ya hizo nyakati za jioni na za asubuhi ambayo yameelezwa ni ya kweli. Lakini uyafiche, kwani ni siri, na bado utapita muda mrefu kabla hayajatimia.’ Biblia Habari Njema - BHND Maono ya hizo nyakati za jioni na za asubuhi ambayo yameelezwa ni ya kweli. Lakini uyafiche, kwani ni siri, na bado utapita muda mrefu kabla hayajatimia.’ Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maono ya hizo nyakati za jioni na za asubuhi ambayo yameelezwa ni ya kweli. Lakini uyafiche, kwani ni siri, na bado utapita muda mrefu kabla hayajatimia.’ Neno: Bibilia Takatifu “Maono kuhusu jioni na asubuhi ambayo umepewa ni kweli, lakini yatie muhuri maono haya, kwa maana yanahusu nyakati za baadaye sana.” Neno: Maandiko Matakatifu “Maono kuhusu jioni na asubuhi ambayo umepewa ni kweli, lakini yatie muhuri maono haya, kwa maana yanahusu wakati mrefu ujao.” Swahili Roehl Bible 1937 Nayo, uliyoyaona ya kuchwa na kucha na kuambiwa habari zao, ni ya kweli. Lakini wewe iandike ndoto hii, kisha iweke kifichoni, kwani ni ya mambo ya siku nyingi. |
nao watakusanywa pamoja kama vile wakusanywavyo wafungwa katika shimo nao watafungwa katika gereza; na baada ya muda wa siku nyingi wataadhibiwa.
Mwanadamu, tazama, hao wa nyumba ya Israeli husema, Maono hayo ayaonayo ni ya siku nyingi zijazo, naye anatabiri habari ya nyakati zilizo mbali sana.
Katika mwaka wa tatu wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, Danieli, ambaye jina lake aliitwa Belteshaza, alifunuliwa neno; na neno lile lilikuwa kweli; maana ni vita vikubwa; naye akalifahamu neno lile, akaelewa na maono hayo.
Sasa nimekuja kukufahamisha mambo yatakayowapata watu wako katika siku za mwisho; maana maono hayo ni ya siku nyingi bado.
Nami sasa nitakuonesha yaliyo kweli. Tazama, watasimama wafalme watatu katika Uajemi; naye mfalme wa nne atakuwa tajiri kuliko hao wote; naye atakapopata nguvu kwa utajiri wake, atawachochea wote juu ya ufalme wa Ugiriki.
Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie mhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huku na huko, na maarifa yataongezeka.
Akasema, Nenda zako, Danieli; maana maneno haya yamefungwa, na kutiwa mhuri, hata wakati wa mwisho.
Na ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nilikuwa tayari kuandika. Nami nilisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Yatie mhuri maneno hayo yaliyonenwa na hizo ngurumo saba, usiyaandike.
Akaniambia, Usiyatie mhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia.