Nikatazama wakati huo; kwa sababu ya sauti ya yale maneno makubwa iliyoyasema ile pembe; nilitazama hata mnyama yule akauawa, mwili wake ukaharibiwa, akatolewa ateketezwe kwa moto.
Danieli 7:12 - Swahili Revised Union Version Na kwa habari za wale wanyama wengine, walinyang'anywa mamlaka yao; lakini maisha yao yalidumishwa kwa wakati na majira. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wale wanyama wengine walinyanganywa mamlaka yao, lakini wao wenyewe wakaachwa waendelee kuishi kwa muda fulani. Biblia Habari Njema - BHND Wale wanyama wengine walinyanganywa mamlaka yao, lakini wao wenyewe wakaachwa waendelee kuishi kwa muda fulani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wale wanyama wengine walinyang'anywa mamlaka yao, lakini wao wenyewe wakaachwa waendelee kuishi kwa muda fulani. Neno: Bibilia Takatifu (Wanyama wengine walikuwa wamevuliwa mamlaka yao, lakini waliruhusiwa kuishi kwa muda.) Neno: Maandiko Matakatifu (Wanyama wengine walikuwa wamevuliwa mamlaka yao, lakini waliruhusiwa kuishi kwa muda fulani.) Swahili Roehl Bible 1937 Kisha nao wale nyama wengine walinyang'anywa nguvu zao za kutawala, kwani walikuwa wamekatiwa wingi wa siku zao za kuwapo, wasipite wala mwaka wala siku. |
Nikatazama wakati huo; kwa sababu ya sauti ya yale maneno makubwa iliyoyasema ile pembe; nilitazama hata mnyama yule akauawa, mwili wake ukaharibiwa, akatolewa ateketezwe kwa moto.
Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye.
Nikamwona akimkaribia kondoo dume, akamwonea hasira kali, akampiga kondoo dume, akazivunja pembe zake mbili; na huyo kondoo dume alikuwa hana nguvu kusimama mbele yake; bali akamwangusha chini, akamkanyagakanyaga; wala hapakuwapo awezaye kumwokoa kondoo dume katika mkono wake.