lakini mambo haya mawili yatakupata katika dakika moja siku moja, kufiwa na watoto, na ujane; yatakupata kiasi kamili, uchawi wako ujapokuwa mwingi, na uganga wako mwingi mno.
Danieli 5:30 - Swahili Revised Union Version Usiku huo huo Belshaza, mfalme wa Wakaldayo, akauawa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usiku huo huo, mfalme Belshaza wa Wakaldayo, aliuawa; Biblia Habari Njema - BHND Usiku huo huo, mfalme Belshaza wa Wakaldayo, aliuawa; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usiku huo huo, mfalme Belshaza wa Wakaldayo, aliuawa; Neno: Bibilia Takatifu Usiku ule ule, Belshaza mfalme wa Wakaldayo akauawa, Neno: Maandiko Matakatifu Usiku ule ule, Belshaza mfalme wa Wakaldayo akauawa, Swahili Roehl Bible 1937 Usiku uleule Belsasari, mfalme wa Wakasidi, akauawa. |
lakini mambo haya mawili yatakupata katika dakika moja siku moja, kufiwa na watoto, na ujane; yatakupata kiasi kamili, uchawi wako ujapokuwa mwingi, na uganga wako mwingi mno.
Nimekutegea mtego, Ee Babeli, nawe ukanaswa, nawe ulikuwa huna habari; umeonekana, ukakamatwa, kwa sababu ulishindana na BWANA.
Inoeni hiyo mishale; zishikeni ngao kwa nguvu; BWANA ameziamsha roho za wafalme wa Wamedi; kwa sababu shauri lake ni juu ya Babeli auangamize; maana ni kisasi cha BWANA, kisasi cha hekalu lake.
Tarishi mmoja atapiga mbio kumlaki mwingine, Na mjumbe mmoja atapiga mbio kumlaki mwenziwe, Ili kumpasha habari mfalme wa Babeli, Ya kuwa mji wake umetwaliwa kila upande.
Wakiingiwa na ukali, nitawafanyia karamu yao, nami nitawalevya, wapate kufurahi, na kulala usingizi wa milele, wasiamke tena, asema BWANA.
Nami nitawalevya wakuu wake, na watu wake wenye hekima, watawala wake, na makamanda wake, na mashujaa wake; nao watalala usingizi wa milele, wasiamke, asema Mfalme, BWANA wa majeshi, ambaye jina lake ni BWANA.
Basi kwa ajili ya hayo sasa watakwenda utumwani pamoja na wa kwanza watakaokwenda utumwani, na kelele za shangwe za hao waliojinyosha zitakoma.