Umewapanda, naam, wametia mizizi, wanakua, naam, wanazaa matunda; katika vinywa vyao u karibu, bali katika mioyo yao u mbali.
Danieli 4:10 - Swahili Revised Union Version Njozi za kichwa changu kitandani mwangu zilikuwa hivi; niliona, na tazama, palikuwa na mti katikati ya nchi, urefu wake mkubwa sana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Nilipokuwa nimelala, niliona maono haya: Niliona mti mrefu sana katikati ya dunia. Biblia Habari Njema - BHND “Nilipokuwa nimelala, niliona maono haya: Niliona mti mrefu sana katikati ya dunia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Nilipokuwa nimelala, niliona maono haya: Niliona mti mrefu sana katikati ya dunia. Neno: Bibilia Takatifu Haya ndio maono niliyoona nilipokuwa nimelala kitandani mwangu: Nilitazama, na mbele yangu ulisimama mti katikati ya nchi. Ulikuwa mrefu sana. Neno: Maandiko Matakatifu Haya ndiyo maono niliyoona nilipokuwa nimelala kitandani mwangu: Nilitazama, na mbele yangu ulisimama mti katikati ya nchi. Ulikuwa mrefu sana. Swahili Roehl Bible 1937 Maono niliyoyaona kwa macho yangu, nilipolala kitandani, ni haya: nilikuwa nikitazama, mara nikaona mti katika nchi, uliokuwa mrefu sana kwa kimo chake. |
Umewapanda, naam, wametia mizizi, wanakua, naam, wanazaa matunda; katika vinywa vyao u karibu, bali katika mioyo yao u mbali.
Nikaota ndoto iliyonitia hofu; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa changu, zikanifadhaisha.
Kisha nikamsikia mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena, Haya maono kuhusu habari ya sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa liletalo ukiwa, yataendelea hata lini, kukanyaga patakatifu na jeshi?