Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Danieli 3:20 - Swahili Revised Union Version

Kisha akawaamuru baadhi ya watu mashujaa wa jeshi lake kuwafunga Shadraka, na Meshaki, na Abednego, na kuwatupa katika lile tanuri lililokuwa likiwaka moto.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Akaamuru watu fulani wenye nguvu kabisa katika jeshi lake wawafunge Shadraki, Meshaki na Abednego na kuwatupa katika ile tanuri ya moto mkali.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Akaamuru watu fulani wenye nguvu kabisa katika jeshi lake wawafunge Shadraki, Meshaki na Abednego na kuwatupa katika ile tanuri ya moto mkali.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Akaamuru watu fulani wenye nguvu kabisa katika jeshi lake wawafunge Shadraki, Meshaki na Abednego na kuwatupa katika ile tanuri ya moto mkali.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

na akawaamuru baadhi ya askari wake wenye nguvu zaidi katika jeshi lake kuwafunga Shadraki, Meshaki na Abednego, na kuwatupa ndani ya tanuru lililowaka moto.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

na kuwaamuru baadhi ya askari wake wenye nguvu zaidi katika jeshi lake kuwafunga Shadraki, Meshaki na Abednego na kuwatupa ndani ya tanuru iwakayo moto.

Tazama sura

Swahili Roehl Bible 1937

Kisha akaagiza watu walio wenye nguvu zaidi katika vikosi vyake, wawafunge akina Sadiraki na Mesaki na Abedi-Nego, kisha wawatupe katika tanuru iwakayo moto.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Danieli 3:20
7 Marejeleo ya Msalaba  

Mkuu wa matowashi akawapa majina; alimwita Danieli, Belteshaza; na Hanania akamwita Shadraka; na Mishaeli akamwita Meshaki; na Azaria akamwita Abednego.


Basi sasa, kama mkiwa tayari wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zumari, na namna zote za ngoma, kuanguka na kuisujudia sanamu niliyoisimamisha, ni vema; bali msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika tanuri liwakalo moto; naye ni nani Mungu yule atakayewaokoa ninyi mikononi mwangu?


Ndipo Nebukadneza akajaa ghadhabu, na sura ya uso wake ikabadilika juu ya Shadraka, na Meshaki, na Abednego, basi akatoa amri watie moto ile tanuri mara saba kuliko desturi yake ya kutiwa moto.


Basi watu hao wakafungwa, wakiwa wamevaa suruali zao, na kanzu zao, na majoho yao, na mavazi yao mengine, wakatupwa katikati ya lile tanuri lililokuwa likiwaka moto.


Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana.


Lakini ilipokuwa karibu usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.