nami nitawarejesha Wamisri walio katika hali ya kufungwa, nami nitawarudisha Pathrosi, nchi ya kuzaliwa kwao; na huko watakuwa ufalme duni.
Danieli 11:42 - Swahili Revised Union Version Naye ataunyosha mkono wake juu ya nchi hizo, hata na nchi ya Misri haitaokoka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakati atakapozivamia nchi hizo, hata nchi ya Misri haitanusurika. Biblia Habari Njema - BHND Wakati atakapozivamia nchi hizo, hata nchi ya Misri haitanusurika. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakati atakapozivamia nchi hizo, hata nchi ya Misri haitanusurika. Neno: Bibilia Takatifu Atapanua mamlaka yake juu ya nchi nyingi; hata Misri haitaepuka. Neno: Maandiko Matakatifu Atapanua mamlaka yake juu ya nchi nyingi; hata Misri haitaepuka. Swahili Roehl Bible 1937 Kisha ataukunjua mkono wake, aziteke hizo nchi; hapo nchi ya Misri nayo haitapata kupona. |
nami nitawarejesha Wamisri walio katika hali ya kufungwa, nami nitawarudisha Pathrosi, nchi ya kuzaliwa kwao; na huko watakuwa ufalme duni.
Tena ataingia katika hiyo nchi ya uzuri, na nchi nyingi zitapinduliwa; lakini nchi hizi zitaokolewa na mkono wake, Edomu, na Moabu, na wakuu wa watu wa Amoni.
Lakini atakuwa na nguvu juu ya hazina za dhahabu na fedha, na juu ya vitu vyote vya Misri vyenye thamani; na Walibya na Wakushi watafuata nyayo zake.
Tena itakuwa, ya kwamba mtu awaye yote wa jamaa zote zilizomo duniani, asiyekwea kwenda Yerusalemu ili kumwabudu Mfalme, BWANA wa majeshi, mvua haitanyesha kwao.
Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu, uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wao aliposulubiwa.