hata kinyume cha hayo, ni afadhali mmsamehe na kumfariji, mtu kama huyo asije akamezwa katika huzuni yake ipitayo kiasi.
2 Wakorintho 2:8 - Swahili Revised Union Version Kwa hiyo nawasihi kumthibitishia upendo wenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa hiyo nawasihi: Mwonesheni kwamba mnampenda. Biblia Habari Njema - BHND Kwa hiyo nawasihi: Mwonesheni kwamba mnampenda. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa hiyo nawasihi: mwonesheni kwamba mnampenda. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo, nawasihi mpate kuuthibitisha tena upendo wenu kwake. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo, nawasihi, mpate kuuthibitisha tena upendo wenu kwa ajili yake. BIBLIA KISWAHILI Kwa hiyo nawasihi kumthibitishia upendo wenu. |
hata kinyume cha hayo, ni afadhali mmsamehe na kumfariji, mtu kama huyo asije akamezwa katika huzuni yake ipitayo kiasi.
Maana niliandika kwa sababu hii pia, ili nipate wazi kwenu kwamba mmekuwa wenye kutii katika mambo yote.
Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.
Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.