Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulika yaliyositirika katika giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.
2 Wakorintho 10:9 - Swahili Revised Union Version nisije nikaonekana kana kwamba nataka kuwaogofya kwa nyaraka zangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sipendi mfikiri kwamba nataka kuwatisha nyinyi kwa barua zangu. Biblia Habari Njema - BHND Sipendi mfikiri kwamba nataka kuwatisha nyinyi kwa barua zangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sipendi mfikiri kwamba nataka kuwatisha nyinyi kwa barua zangu. Neno: Bibilia Takatifu Sitaki nionekane kama ninayejaribu kuwatisha kwa nyaraka zangu. Neno: Maandiko Matakatifu Sitaki nionekane kama ninayejaribu kuwatisha kwa nyaraka zangu. BIBLIA KISWAHILI nisije nikaonekana kana kwamba nataka kuwaogofya kwa nyaraka zangu. |
Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulika yaliyositirika katika giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.
Maana wasema, Nyaraka zake ni nzito, hodari; bali akiwapo mwenyewe mwilini ni dhaifu, na maneno yake si kitu.
Maana, nijapojisifu zaidi kidogo kwa ajili ya mamlaka yetu, (tuliyopewa na Bwana, tupate kuwajenga wala si kuwaangusha), sitatahayarika;