Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu yeyote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha.
2 Wafalme 7:11 - Swahili Revised Union Version Na mabawabu wakaita wakawaambia watu wa nyumba ya mfalme. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Walinda malango wakaeneza habari hizi mpaka zikafika nyumbani kwa mfalme. Biblia Habari Njema - BHND Walinda malango wakaeneza habari hizi mpaka zikafika nyumbani kwa mfalme. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Walinda malango wakaeneza habari hizi mpaka zikafika nyumbani kwa mfalme. Neno: Bibilia Takatifu Walinzi wa langoni wakatangaza habari ile kwa sauti kuu, na taarifa hii ikatolewa ndani ya jumba la mfalme. Neno: Maandiko Matakatifu Walinzi wa langoni wakatangaza habari ile kwa sauti kuu, na taarifa hii ikatolewa ndani ya jumba la mfalme. BIBLIA KISWAHILI Na mabawabu wakaita, wakawaambia watu wa nyumba ya mfalme. |
Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu yeyote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha.
Mfalme akaondoka usiku, akawaambia watumishi wake, Sasa nitawaonesha ninyi walivyotutendea Washami. Wanajua ya kuwa tuna njaa; basi wametoka kituoni, ili kujificha shambani, wakisema Watakapotoka mjini, tutawakamata hai; tena tutapata kuingia mjini.