Ikawa, walipoona ya kuwa fedha nyingi imo kashani, karani wa mfalme akapanda na kuhani mkuu, wakaifunga mifukoni, wakaihesabu fedha iliyoonekana nyumbani mwa BWANA.
2 Wafalme 22:3 - Swahili Revised Union Version Ikawa, katika mwaka wa kumi na nane wa mfalme Yosia, mfalme akamtuma Shafani, mwana wa Azalia, mwana wa Meshulamu, mwandishi, nyumbani kwa Bwana, akisema, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wake, mfalme alimtuma katibu Shafani, mwana wa Azalia, mwana wa Meshulamu, katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu akisema, Biblia Habari Njema - BHND Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wake, mfalme alimtuma katibu Shafani, mwana wa Azalia, mwana wa Meshulamu, katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu akisema, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wake, mfalme alimtuma katibu Shafani, mwana wa Azalia, mwana wa Meshulamu, katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu akisema, Neno: Bibilia Takatifu Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wake, Mfalme Yosia akamtuma mwandishi Shafani mwana wa Azalia, mwana wa Meshulamu, kwenda katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. Akasema: Neno: Maandiko Matakatifu Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wake, Mfalme Yosia akamtuma mwandishi Shafani mwana wa Azalia, mwana wa Meshulamu, kwenda katika Hekalu la bwana. Akasema: BIBLIA KISWAHILI Ikawa, katika mwaka wa kumi na nane wa mfalme Yosia, mfalme akamtuma Shafani, mwana wa Azalia, mwana wa Meshulamu, mwandishi, nyumbani kwa Bwana, akisema, |
Ikawa, walipoona ya kuwa fedha nyingi imo kashani, karani wa mfalme akapanda na kuhani mkuu, wakaifunga mifukoni, wakaihesabu fedha iliyoonekana nyumbani mwa BWANA.
Bali katika mwaka wa kumi na nane wa mfalme Yosia ilifanyika Pasaka hii kwa BWANA ndani ya Yerusalemu.
ambaye neno la BWANA lilimjia katika siku za Yosia, mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda, katika mwaka wa kumi na tatu wa kutawala kwake.
Basi, wakati huo Baruku akayasoma maneno ya Yeremia katika nyumba ya BWANA, katika chumba cha Gemaria, mwana wa Shafani, mwandishi, katika ua wa juu, mahali pa kuingilia kwa lango jipya la nyumba ya BWANA, akiyasoma katika masikio ya watu wote.
Basi, Mikaya, mwana wa Gemaria, mwana wa Shafani, aliposikia maneno yote ya BWANA yaliyokuwa katika kitabu hicho,
akashuka, akaingia katika nyumba ya mfalme, katika chumba cha mwandishi, na, tazama, wakuu wote wameketi humo, nao ni hawa, Elishama, mwandishi, na Delaya, mwana wa Shemaya, na Elnathani, mwana wa Akbori, na Gemaria, mwana wa Shafani, na Sedekia, mwana wa Hanania, na wakuu wote.