Katika mwaka wa saba wa Yehu, Yoashi alianza kutawala; akatawala miaka arubaini huko Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Sibia wa Beer-sheba.
2 Wafalme 12:2 - Swahili Revised Union Version Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA siku zake zote Yehoyada kuhani alizomfundisha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakati wa maisha yake yote alitenda mema mbele ya Mwenyezi-Mungu, kwa sababu kuhani Yehoyada alikuwa akimfundisha. Biblia Habari Njema - BHND Wakati wa maisha yake yote alitenda mema mbele ya Mwenyezi-Mungu, kwa sababu kuhani Yehoyada alikuwa akimfundisha. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakati wa maisha yake yote alitenda mema mbele ya Mwenyezi-Mungu, kwa sababu kuhani Yehoyada alikuwa akimfundisha. Neno: Bibilia Takatifu Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu miaka yote ambayo Yehoyada kuhani alikuwa akimwelekeza. Neno: Maandiko Matakatifu Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa bwana miaka yote ambayo Yehoyada kuhani alikuwa akimwelekeza. BIBLIA KISWAHILI Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA siku zake zote Yehoyada kuhani alizomfundisha. |
Katika mwaka wa saba wa Yehu, Yoashi alianza kutawala; akatawala miaka arubaini huko Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Sibia wa Beer-sheba.
Ila mahali pa juu hapakuondolewa; watu wakaendelea kutoa sadaka na kufukiza uvumba katika mahali pa juu.
Ndipo mfalme Yoashi akamwita Yehoyada kuhani, na makuhani wengine, akawauliza, Mbona hamtengenezi mabomoko ya nyumba? Basi sasa msipokee tena fedha kwa hao mwajuao, lakini itoeni kwa ajili ya mabomoko ya nyumba.
Akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA, ila si kama babaye Daudi; akafanya kama yote aliyoyafanya baba yake Yoashi.