Na wana watatu wa Seruya walikuwako huko, Yoabu, na Abishai, na Asaheli; na Asaheli alikuwa mwepesi wa miguu kama kulungu.
2 Samueli 2:19 - Swahili Revised Union Version Naye Asaheli akamfuatia Abneri; na katika kwenda kwake hakugeuka kwenda mkono wa kulia wala mkono wa kushoto katika kumfuatia Abneri. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Asaheli alimfuatia Abneri moja kwa moja bila kugeuka kulia wala kushoto. Biblia Habari Njema - BHND Asaheli alimfuatia Abneri moja kwa moja bila kugeuka kulia wala kushoto. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Asaheli alimfuatia Abneri moja kwa moja bila kugeuka kulia wala kushoto. Neno: Bibilia Takatifu Asaheli akamfukuza Abneri, pasipo kugeuka kulia wala kushoto wakati alimfuata. Neno: Maandiko Matakatifu Asaheli akamfukuza Abneri, pasipo kugeuka kulia wala kushoto wakati akimfuata. BIBLIA KISWAHILI Naye Asaheli akamfuatia Abneri; na katika kwenda kwake hakugeuka kwenda mkono wa kulia wala mkono wa kushoto katika kumfuatia Abneri. |
Na wana watatu wa Seruya walikuwako huko, Yoabu, na Abishai, na Asaheli; na Asaheli alikuwa mwepesi wa miguu kama kulungu.
Basi Abneri akamwambia, Geuka mkono wa kulia au mkono wa kushoto, ukamshike mmoja wa vijana, ukazitwae silaha zake. Lakini Asaheli hakukubali kugeuka na kuacha kumfuata.
Basi Abneri alipokuwa amerudi Hebroni, Yoabu akamchukua kando hadi katikati ya lango, ili aseme naye kwa faragha; akampiga mkuki wa tumbo huko, hadi akafa; kwa ajili ya damu ya Asaheli, ndugu yake.
Basi Yoabu, na Abishai nduguye, walimwua Abneri, kwa sababu yeye alimwua ndugu yao Asaheli katika vita huko Gibeoni.
Akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA, akaenda katika njia yote ya Daudi baba yake, wala hakugeuka upande wa kulia wala wa kushoto.
Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda kulingana na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kulia, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.
Basi, iweni thabiti sana kuyashika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Torati ya Musa, na kuyatenda, msiyaache kwa kugeukia upande wa kulia wala upande wa kushoto.