Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

2 Samueli 19:41 - Swahili Revised Union Version

Tena, angalia, watu wote wa Israeli wakamjia mfalme wakamwambia mfalme, Kwa nini ndugu zetu, watu wa Yuda wamekuiba, na kumvusha Yordani mfalme, na jamaa yake, na watu wote wa Daudi pamoja naye?

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Kisha, watu wote wa Israeli wakaja kwa mfalme na kumwambia, “Kwa nini ndugu zetu watu wa Yuda walikuwa wamekuiba ukiwa njiani, wakakuvusha mto Yordani, wewe na jamaa yako, pamoja na watu wako?”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Kisha, watu wote wa Israeli wakaja kwa mfalme na kumwambia, “Kwa nini ndugu zetu watu wa Yuda walikuwa wamekuiba ukiwa njiani, wakakuvusha mto Yordani, wewe na jamaa yako, pamoja na watu wako?”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Kisha, watu wote wa Israeli wakaja kwa mfalme na kumwambia, “Kwa nini ndugu zetu watu wa Yuda walikuwa wamekuiba ukiwa njiani, wakakuvusha mto Yordani, wewe na jamaa yako, pamoja na watu wako?”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Baada ya kitambo kidogo, wanaume wote wa Israeli wakaja kwa mfalme na kumwambia, “Kwa nini ndugu zetu, wanaume wa Yuda, wamemrudisha mfalme kwa siri bila kutushirikisha, na kumvusha ng’ambo ya Yordani, yeye na nyumba yake, pamoja na watu wake wote?”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Baada ya kitambo kidogo watu wote wa Israeli wakaja kwa mfalme na kumwambia, “Kwa nini ndugu zetu, watu wa Yuda, wamemrudisha mfalme kwa siri bila kutushirikisha, na kumvusha ng’ambo ya Yordani, yeye na nyumba yake, pamoja na watu wake wote?”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Tena, angalia, watu wote wa Israeli wakamjia mfalme wakamwambia mfalme, Kwa nini ndugu zetu, watu wa Yuda wamekuiba, na kumvusha Yordani mfalme, na jamaa yake, na watu wote wa Daudi pamoja naye?

Tazama sura
Tafsiri zingine

2 Samueli 19:41
7 Marejeleo ya Msalaba  

Naye mfalme Daudi akatuma kwa Sadoki na Abiathari, makuhani, kusema, Neneni na wazee wa Yuda, mkisema, Kwa nini ninyi mmekuwa wa mwisho wa kumrudisha tena mfalme nyumbani kwake? Kwa maana maneno ya Israeli wote yamemjia mfalme, ili kumleta nyumbani kwake.

Ninyi ni ndugu zangu, ninyi ni mfupa wangu na nyama yangu; mbona basi ninyi mmekuwa wa mwisho wa kumrudisha tena mfalme?

Watu wakajificha siku ile, wakaingia mjini kama vile watu waonao fedheha wajifichavyo, hapo wakimbiapo vitani.

Kisha watu wa Efraimu walikusanyika na kuvuka hadi Zafoni; wakamwambia Yeftha, Kwa nini ulivuka kwenda kupigana na wana wa Amoni, nawe hukutuita sisi kwenda pamoja nawe? Tutaichoma nyumba yako juu yako.

Basi watu wa Efraimu wakamwambia, Kwa nini umetutendea haya? Hata usituite hapo ulipokwenda kupigana na Wamidiani? Nao wakamshutumu vikali.