Mfalme akauliza, Je! Yule kijana, Absalomu, yuko salama? Ahimaasi akajibu, Yoabu aliponituma mimi mtumishi wa mfalme, mimi mtumishi wako, niliona kishindo kikubwa, lakini sikujua sababu yake.
2 Samueli 18:30 - Swahili Revised Union Version Naye mfalme akasema, Geuka, usimame hapa. Akageuka, akasimama. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mfalme akasema, “Kaa kando, na usimame hapo.” Basi, Ahimaasi akaenda kando na kusimama kimya. Biblia Habari Njema - BHND Mfalme akasema, “Kaa kando, na usimame hapo.” Basi, Ahimaasi akaenda kando na kusimama kimya. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mfalme akasema, “Kaa kando, na usimame hapo.” Basi, Ahimaasi akaenda kando na kusimama kimya. Neno: Bibilia Takatifu Mfalme akasema, “Simama kando na usubiri hapa.” Basi akasogea kando na kusimama hapo. Neno: Maandiko Matakatifu Mfalme akasema, “Simama kando na usubiri hapa.” Basi akasogea kando na kusimama hapo. BIBLIA KISWAHILI Naye mfalme akasema, Geuka, usimame hapa. Akageuka, akasimama. |
Mfalme akauliza, Je! Yule kijana, Absalomu, yuko salama? Ahimaasi akajibu, Yoabu aliponituma mimi mtumishi wa mfalme, mimi mtumishi wako, niliona kishindo kikubwa, lakini sikujua sababu yake.
Na tazama, yule Mkushi akafika; Mkushi akasema, Nina habari kwa bwana wangu mfalme; kwa maana BWANA amekulipizia kisasi leo juu ya hao wote walioinuka kupigana nawe.