Lakini Absalomu akakimbia. Na kijana yule aliyekuwa mlinzi akainua macho yake, akaona, na tazama, kuna watu wengi wanakuja kwa njia ya upande wa kilima nyuma yake.
2 Samueli 13:38 - Swahili Revised Union Version Basi Absalomu akakimbia, akaenda Geshuri, akakaa huko muda wa miaka mitatu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Absalomu alikimbilia mjini Geshuri, akakaa huko kwa muda wa miaka mitatu. Biblia Habari Njema - BHND Absalomu alikimbilia mjini Geshuri, akakaa huko kwa muda wa miaka mitatu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Absalomu alikimbilia mjini Geshuri, akakaa huko kwa muda wa miaka mitatu. Neno: Bibilia Takatifu Baada ya Absalomu kukimbia na kwenda Geshuri, akakaa huko miaka mitatu. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya Absalomu kukimbia na kwenda Geshuri, akakaa huko miaka mitatu. BIBLIA KISWAHILI Basi Absalomu akakimbia, akaenda Geshuri, akakaa huko muda wa miaka mitatu. |
Lakini Absalomu akakimbia. Na kijana yule aliyekuwa mlinzi akainua macho yake, akaona, na tazama, kuna watu wengi wanakuja kwa njia ya upande wa kilima nyuma yake.
Mwanamke akasema, Kwa nini basi wewe umewafikiria mambo kama hayo watu wa Mungu? Maana kwa kunena neno hili mfalme ni kama mwenye hatia, kwa kuwa hamrudishi kwao tena yule mfukuzwa wake.
Absalomu akamjibu Yoabu, Angalia, nilituma kwako, nikisema, Njoo kwangu, ili nikutume kwa mfalme kunena, Mbona nimekuja kutoka Geshuri? Ingekuwa heri kwangu kama ningekuwako huko hata sasa; basi sasa na nimtazame uso mfalme; na ukiwapo uovu kwangu, na aniue.
Maana mimi mtumishi wako niliweka nadhiri hapo nilipokuwa nikikaa Geshuri katika Shamu, nikasema, Kama BWANA akinirudisha Yerusalemu kweli, ndipo nitamtumikia BWANA.
na wa pili wake Danieli, wa Abigaili mkewe Nabali wa Karmeli; na wa tatu Absalomu, mwana wa Maaka binti Talmai, mfalme wa Geshuri,