Naomba, warudishieni hivi leo mashamba yao, mashamba yao ya mizabibu, mashamba yao ya mizeituni, nyumba zao, lile fungu la mia la fedha, la ngano, la divai, na la mafuta, mnalowatoza.
2 Samueli 12:6 - Swahili Revised Union Version naye atamrudishia yule mwana-kondoo mara nne, kwa sababu ametenda neno hili, na kwa sababu hakuwa na huruma. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ni lazima amlipe yule maskini mwanakondoo huyo, tena mara nne, kwani ametenda jambo baya na hakuwa na huruma!” Biblia Habari Njema - BHND Ni lazima amlipe yule maskini mwanakondoo huyo, tena mara nne, kwani ametenda jambo baya na hakuwa na huruma!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ni lazima amlipe yule maskini mwanakondoo huyo, tena mara nne, kwani ametenda jambo baya na hakuwa na huruma!” Neno: Bibilia Takatifu Lazima alipe mara nne zaidi, kwa ajili ya kondoo huyo, kwa sababu amefanya jambo kama hilo na hakuwa na huruma.” Neno: Maandiko Matakatifu Lazima alipe mara nne zaidi, kwa ajili ya kondoo huyo, kwa sababu amefanya jambo kama hilo na hakuwa na huruma.” BIBLIA KISWAHILI naye atamrudishia yule mwana-kondoo mara nne, kwa sababu ametenda neno hili, na kwa sababu hakuwa na huruma. |
Naomba, warudishieni hivi leo mashamba yao, mashamba yao ya mizabibu, mashamba yao ya mizeituni, nyumba zao, lile fungu la mia la fedha, la ngano, la divai, na la mafuta, mnalowatoza.
mwenye shimo atalipa; atampa huyo mwenye mnyama fedha, na mnyama aliyekufa atakuwa ni wake.
Mtu akiiba ng'ombe au kondoo, na kumchinja, au kumwuza; atalipa ng'ombe watano badala ya ng'ombe mmoja, na kondoo wanne badala ya kondoo mmoja.
au kitu chochote ambacho amekiapia uongo; atakirudisha hata kwa utimilifu wake, kisha ataongeza na sehemu ya tano zaidi juu yake; naye atampa huyo mwenyewe, siku hiyo ambayo atakapohukumiwa kuwa mwenye hatia.
Zakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana, nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang'anya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne.