Akasema, Wakiwa Washami hodari mno kwangu, ndipo wewe utanisaidia, lakini Waamoni wakiwa ni hodari mno kwako, ndipo mimi nitakuja nikusaidie wewe.
2 Samueli 10:10 - Swahili Revised Union Version akawatia nguvu watu waliosalia mkononi mwa Abishai, nduguye, akawapanga juu ya Waamoni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wale wanajeshi wengine waliobaki aliwaweka chini ya uongozi wa ndugu yake Abishai, naye akawapanga ili wakabiliane na Waamoni. Biblia Habari Njema - BHND Wale wanajeshi wengine waliobaki aliwaweka chini ya uongozi wa ndugu yake Abishai, naye akawapanga ili wakabiliane na Waamoni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wale wanajeshi wengine waliobaki aliwaweka chini ya uongozi wa ndugu yake Abishai, naye akawapanga ili wakabiliane na Waamoni. Neno: Bibilia Takatifu Akawaweka waliobaki chini ya uongozi wa Abishai nduguye na kuwapanga dhidi ya Waamoni. Neno: Maandiko Matakatifu Akawaweka waliobaki chini ya uongozi wa Abishai nduguye na kuwapanga dhidi ya Waamoni. BIBLIA KISWAHILI akawatia nguvu watu waliosalia mkononi mwa Abishai, nduguye, akawapanga juu ya Waamoni. |
Akasema, Wakiwa Washami hodari mno kwangu, ndipo wewe utanisaidia, lakini Waamoni wakiwa ni hodari mno kwako, ndipo mimi nitakuja nikusaidie wewe.
Basi Yoabu alipoona ya kwamba uso wa vita umekuwa juu yake mbele na nyuma, akachagua baadhi ya wateule wote wa Israeli, akawapanga juu ya Washami;
Daudi akawatuma hao watu vitani, theluthi moja chini ya mkono wa Yoabu, na theluthi ya pili chini ya mkono wa Abishai, mwana wa Seruya nduguye Yoabu, na theluthi ya tatu chini ya mkono wa Itai, Mgiti. Mfalme akawaambia watu, Bila shaka mimi mwenyewe nami nitatoka pamoja nanyi.
Tena, Abishai, nduguye Yoabu, mwana wa Seruya, alikuwa mkuu wa wale watatu. Huyo aliuinua mkuki wake juu ya watu mia tatu, akawaua, akawa na jina kati ya wale watatu.
Tena Abishai, mwana wa Seruya, akawaua Waedomi elfu kumi na nane katika Bonde la Chumvi.
Ikawa baada ya hayo, Nahashi, mfalme wa wana wa Amoni, akafa, akatawala mwanawe mahali pake.