Walio fahari yako, Ee Israeli Juu ya mahali pako palipoinuka wameuawa; Jinsi mashujaa walivyoanguka!
2 Samueli 1:27 - Swahili Revised Union Version Jinsi mashujaa walivyoanguka, Na silaha za vita zilivyoangamia! Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Jinsi gani mashujaa wameanguka, na silaha zao zimeachwa, hazina kazi.” Biblia Habari Njema - BHND “Jinsi gani mashujaa wameanguka, na silaha zao zimeachwa, hazina kazi.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Jinsi gani mashujaa wameanguka, na silaha zao zimeachwa, hazina kazi.” Neno: Bibilia Takatifu “Tazama jinsi mashujaa walivyoanguka! Silaha za vita zimeangamia!” Neno: Maandiko Matakatifu “Tazama jinsi mashujaa walivyoanguka! Silaha za vita zimeangamia!” BIBLIA KISWAHILI Jinsi mashujaa walivyoanguka, Na silaha za vita zilivyoangamia! |
Walio fahari yako, Ee Israeli Juu ya mahali pako palipoinuka wameuawa; Jinsi mashujaa walivyoanguka!
Jinsi mashujaa walivyoanguka Katikati ya vita! Ee Yonathani, wewe umeuawa Juu ya mahali pako palipoinuka.
Basi Elisha alikuwa ameshikwa na ugonjwa wake uliomwua; naye Yehoashi mfalme wa Israeli akateremka amtazame, akamlilia mbele yake, akasema, Baba yangu! Baba yangu! Gari la Israeli na wapanda farasi wake!
Naye Elisha akaona, akalia, Baba yangu, baba yangu, gari la Israeli na wapanda farasi wake! Asimwone tena kabisa; akashika mavazi yake mwenyewe, akayararua vipande viwili.
watu waliotoka katika nchi iliyo mbali, tokea upande wa mwisho wa mbingu; naam, BWANA na silaha za ghadhabu yake, ili aiangamize nchi yote.