Enyi binti za Israeli, mlilieni Huyo Sauli, ambaye aliwavika Mavazi mekundu kwa anasa, Akazipamba nguo zenu dhahabu.
2 Samueli 1:23 - Swahili Revised Union Version Sauli na Yonathani walipendwa na kupendeza Maishani wala mautini hawakutengwa; Walikuwa wepesi kuliko tai, Walikuwa hodari kuliko simba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Shauli na Yonathani, watu wa ajabu na wakupendeza. Maishani na kifoni hawakutengana. Walikuwa wepesi kuliko tai, naam, wenye nguvu kuliko simba. Biblia Habari Njema - BHND “Shauli na Yonathani, watu wa ajabu na wakupendeza. Maishani na kifoni hawakutengana. Walikuwa wepesi kuliko tai, naam, wenye nguvu kuliko simba. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Shauli na Yonathani, watu wa ajabu na wakupendeza. Maishani na kifoni hawakutengana. Walikuwa wepesi kuliko tai, naam, wenye nguvu kuliko simba. Neno: Bibilia Takatifu Sauli na Yonathani: maishani walipendwa na kuneemeka, na katika kifo hawakutengana. Walikuwa wepesi kuliko tai, walikuwa na nguvu kuliko simba. Neno: Maandiko Matakatifu “Sauli na Yonathani, maishani walipendwa na kuneemeka, na katika kifo hawakutengana. Walikuwa wepesi kuliko tai, walikuwa na nguvu kuliko simba. BIBLIA KISWAHILI Sauli na Yonathani walipendwa na kupendeza Maishani wala mautini hawakutengwa; Walikuwa wepesi kuliko tai, Walikuwa hodari kuliko simba. |
Enyi binti za Israeli, mlilieni Huyo Sauli, ambaye aliwavika Mavazi mekundu kwa anasa, Akazipamba nguo zenu dhahabu.
Na wana watatu wa Seruya walikuwako huko, Yoabu, na Abishai, na Asaheli; na Asaheli alikuwa mwepesi wa miguu kama kulungu.
Tena Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari wa Kabseeli aliyekuwa amefanya mambo makuu; aliwaua simba wawili wakali wa Moabu, pia aliingia katika shimo na kumwua simba wakati wa theluji;
Na wa Wagadi wakajitenga kumfuata Daudi ngomeni huko nyikani, wanaume mashujaa, watu waliozoea vita, walioweza kutumia ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kama nyuso za simba, nao walikuwa wepesi kama kulungu juu ya milima;
Kinywa chake kimejaa maneno matamu, Ndiye mzuri sana kwa ujumla. Ni huyu mpendwa wangu, ni huyu rafiki yangu, Enyi binti za Yerusalemu.
Tazama atapanda juu kama mawingu, na magari yake ya vita yatakuwa kama kisulisuli; farasi wake ni wepesi kuliko tai. Ole wetu, kwa sababu tumeharibika.
Waliotufuatia ni wepesi Kuliko tai za mbinguni; Hao walitufuatia milimani, Nao walituotea jangwani.
BWANA atakuletea taifa juu yako kutoka mbali, kutoka ncha ya dunia, kama arukavyo tai; taifa usiloufahamu ulimi wake;
Nao watu wa mji wakamwambia siku ya saba kabla ya jua kuchwa, Ni kitu gani kilicho tamu kuliko asali? Ni kitu gani kilicho na nguvu kuliko simba? Naye akawaambia, Msingelima na mtamba wangu, Hamngekitegua kitendawili changu.
Ikawa Daudi alipokwisha kusema na Sauli, roho ya Yonathani, ikaambatana na roho ya Daudi, Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe.
Naye akamwambia, Hasha! Hutakufa; angalia, baba yangu hatendi neno kubwa wala dogo bila kunifunulia, na baba yangu ana sababu gani ya kunificha jambo hili? Sivyo usemavyo.