Nao waliokaa katika nchi, wale Wakanaani, walipoyaona matanga katika sakafu ya Atadi, wakasema, Matanga haya ya Wamisri ni makuu kwa hiyo mahali pale paliitwa Abel-Misri, iliyo ng'ambo ya Yordani.
2 Samueli 1:17 - Swahili Revised Union Version Basi Daudi akamwomboleza Sauli, na Yonathani, mwanawe, maombolezo haya; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Daudi aliimba ombolezo lifuatalo kwa ajili ya Shauli na mwanawe Yonathani. Biblia Habari Njema - BHND Daudi aliimba ombolezo lifuatalo kwa ajili ya Shauli na mwanawe Yonathani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Daudi aliimba ombolezo lifuatalo kwa ajili ya Shauli na mwanawe Yonathani. Neno: Bibilia Takatifu Daudi akafanya maombolezo haya kuhusu Sauli na Yonathani mwanawe, Neno: Maandiko Matakatifu Daudi akafanya maombolezo haya kuhusu Sauli na Yonathani mwanawe, BIBLIA KISWAHILI Basi Daudi akamwombolezea Sauli, na Yonathani, mwanawe, maombolezo haya; |
Nao waliokaa katika nchi, wale Wakanaani, walipoyaona matanga katika sakafu ya Atadi, wakasema, Matanga haya ya Wamisri ni makuu kwa hiyo mahali pale paliitwa Abel-Misri, iliyo ng'ambo ya Yordani.
Walio fahari yako, Ee Israeli Juu ya mahali pako palipoinuka wameuawa; Jinsi mashujaa walivyoanguka!
Naye Yeremia akamlilia Yosia; na waimbaji wote wanaume kwa wawanawake wakamtaja Yosia katika maombolezo yao, hadi leo; hata wakayafanya kuwa ada kwa Israeli; nayo, tazama, yameandikwa katika Maombolezo.
Nilisikitika kana kwamba ni rafiki au ndugu yangu, Niliinama nikilia kama aliyefiwa na mamaye.
Hayo ndiyo maombolezo watakayoimba; binti za mataifa watayaimba; kwa hayo wataomboleza kwa ajili ya Misri, na kwa ajili ya watu wake umati wote, asema Bwana MUNGU.