Tazama, hivi ni viunga tu vya njia zake; Na jinsi yalivyo madogo manong'ono tusikiayo katika habari zake! Lakini ngurumo za uweza wake ni nani awezaye kuzielewa?
1 Wakorintho 13:9 - Swahili Revised Union Version Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana ujuzi wetu si kamili, na kipaji chetu cha kutangaza neno la Mungu si kamili. Biblia Habari Njema - BHND Maana ujuzi wetu si kamili, na kipaji chetu cha kutangaza neno la Mungu si kamili. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana ujuzi wetu si kamili, na kipaji chetu cha kutangaza neno la Mungu si kamili. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana tunafahamu kwa sehemu na tunatoa unabii kwa sehemu. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana tunafahamu kwa sehemu na tunatoa unabii kwa sehemu. BIBLIA KISWAHILI Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu; |
Tazama, hivi ni viunga tu vya njia zake; Na jinsi yalivyo madogo manong'ono tusikiayo katika habari zake! Lakini ngurumo za uweza wake ni nani awezaye kuzielewa?
Ee BWANA, Mungu wangu, umefanya kwa wingi Miujiza yako na mawazo yako kwetu; Hakuna awezaye kufananishwa nawe; Kama ningependa kuyatangaza na kuyahubiri, Ni mengi sana hayahesabiki.
Ni nani aliyepanda mbinguni na kushuka chini? Ni nani aliyekamata upepo kwa makonzi yake? Ni nani aliyeyafunga maji ndani ya nguo yake? Ni nani aliyefanya imara ncha zote za nchi? Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe, kama wajua?
Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na yeyote ambaye Mwana apenda kumfunulia.
Maana sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.
Lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.
Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nilipewa neema hii ya kuwahubiria Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;
Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini tunajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo.