nami nimemjaza Roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina,
1 Wakorintho 12:4 - Swahili Revised Union Version Basi kuna karama tofauti; bali Roho ni yeye yule. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Vipaji vya kiroho ni vya namna nyingi, lakini Roho avitoaye ni mmoja. Biblia Habari Njema - BHND Vipaji vya kiroho ni vya namna nyingi, lakini Roho avitoaye ni mmoja. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Vipaji vya kiroho ni vya namna nyingi, lakini Roho avitoaye ni mmoja. Neno: Bibilia Takatifu Kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni yule yule. Neno: Maandiko Matakatifu Kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni yule yule. BIBLIA KISWAHILI Basi kuna karama tofauti; bali Roho ni yeye yule. |
nami nimemjaza Roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina,
Na Mungu ameweka wengine katika kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, aina za usaidizi, maongozi na aina za lugha.
Ila nipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo; lakini kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi.
Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;
Mungu naye akishuhudia pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa karama za Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.
kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.