Lakini, ndugu zangu, sipendi msiwe na habari, ya kuwa mara nyingi nilikusudia kuja kwenu, nikazuiliwa mpaka sasa, ili nipate kuwa na matunda kwenu ninyi pia kama nilivyo nayo katika Mataifa wengine.
1 Wakorintho 12:1 - Swahili Revised Union Version Basi, ndugu zangu, kuhusu karama za roho, sitaki mkose kufahamu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ndugu, kuhusu vipaji vya kiroho, napenda mfahamu vizuri mambo haya: Biblia Habari Njema - BHND Ndugu, kuhusu vipaji vya kiroho, napenda mfahamu vizuri mambo haya: Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ndugu, kuhusu vipaji vya kiroho, napenda mfahamu vizuri mambo haya: Neno: Bibilia Takatifu Basi ndugu zangu, kuhusu karama za rohoni, sitaki mkose kufahamu. Neno: Maandiko Matakatifu Basi ndugu zangu, kuhusu karama za rohoni, sitaki mkose kufahamu. BIBLIA KISWAHILI Basi, ndugu zangu, kuhusu karama za roho, sitaki mkose kufahamu. |
Lakini, ndugu zangu, sipendi msiwe na habari, ya kuwa mara nyingi nilikusudia kuja kwenu, nikazuiliwa mpaka sasa, ili nipate kuwa na matunda kwenu ninyi pia kama nilivyo nayo katika Mataifa wengine.
Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;
Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana.
Maana ndugu, hatupendi, msijue habari ya dhiki ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hata tukakata tamaa ya kuishi.
Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;
Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.
Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.