1 Wafalme 15:8 - Swahili Revised Union Version Abiya akalala na baba zake, wakamzika mjini mwa Daudi. Akatawala Asa mwanawe mahali pake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwishowe, Abiya alifariki na kuzikwa katika mji wa Daudi na mwanawe Asa akatawala mahali pake. Biblia Habari Njema - BHND Mwishowe, Abiya alifariki na kuzikwa katika mji wa Daudi na mwanawe Asa akatawala mahali pake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwishowe, Abiya alifariki na kuzikwa katika mji wa Daudi na mwanawe Asa akatawala mahali pake. Neno: Bibilia Takatifu Naye Abiya akalala na baba zake akazikwa katika Mji wa Daudi. Asa mwanawe akawa mfalme baada yake. Neno: Maandiko Matakatifu Naye Abiya akalala na baba zake akazikwa katika Mji wa Daudi. Asa mwanawe akawa mfalme baada yake. BIBLIA KISWAHILI Abiya akalala na baba zake, wakamzika mjini mwa Daudi. Akatawala Asa mwanawe mahali pake. |
Rehoboamu akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze mjini mwa Daudi. Na jina la mamaye aliitwa Naama, Mwamoni. Na mwanawe, Abiya, alitawala mahali pake.
Na wazawa wa Sulemani walikuwa: Rehoboamu mwanawe; mwanawe huyo alikuwa Abiya; na mwanawe huyo ni Asa; na mwanawe huyo ni Yehoshafati;
Basi Abiya akalala na baba zake, wakamzika mjini mwa Daudi, akatawala Asa mwanawe mahali pake; katika siku zake nchi ikastarehe miaka kumi.