Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

1 Samueli 6:7 - Swahili Revised Union Version

Basi sasa jifanyieni gari jipya, mtwae na ng'ombe wake wawili wakamwao, ambao hawajafungwa nira, nanyi mkawafunge hao ng'ombe garini, na kuwaondoa ndama wao na kuwatia zizini;

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Basi, tayarisheni gari jipya na ng'ombe wawili wakamuliwao ambao bado hawajafungwa nira; wafungeni kwenye gari hilo lakini ndama wao wasiende pamoja nao, ila wabaki zizini.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Basi, tayarisheni gari jipya na ng'ombe wawili wakamuliwao ambao bado hawajafungwa nira; wafungeni kwenye gari hilo lakini ndama wao wasiende pamoja nao, ila wabaki zizini.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Basi, tayarisheni gari jipya na ng'ombe wawili wakamuliwao ambao bado hawajafungwa nira; wafungeni kwenye gari hilo lakini ndama wao wasiende pamoja nao, ila wabaki zizini.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

“Sasa basi, wekeni gari jipya la kukokotwa pamoja na ng’ombe wawili ambao wamezaa lakini ambao kamwe hawajafungwa nira. Fungieni hao ng’ombe hilo gari, lakini ondoeni ndama wao na mwaweke zizini.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

“Sasa basi, wekeni gari jipya la kukokotwa pamoja na ng’ombe wawili ambao wamezaa lakini ambao kamwe hawajafungwa nira. Fungieni hao ng’ombe hilo gari, lakini ondoeni ndama wao na mwaweke zizini.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Basi sasa jifanyieni gari jipya, mtwae na ng'ombe wake wawili wakamuliwao, ambao hawajafungwa nira, nanyi mkawafunge hao ng'ombe garini, na kuwaondoa ndama wao na kuwatia zizini;

Tazama sura
Tafsiri zingine

1 Samueli 6:7
5 Marejeleo ya Msalaba  

Wakaliweka sanduku la Mungu juu ya gari jipya, wakalitoa katika nyumba ya Abinadabu, iliyoko kilimani; nao Uza na Ahio wana wa Abinadabu wakaliendesha lile gari jipya.

Wakalipandisha sanduku la Mungu juu ya gari jipya kutoka nyumba ya Abinadabu; na Uza na Ahio wakaliendesha lile gari.

Hii ndiyo amri ya sheria BWANA aliyoagiza, akisema, Waambie wana wa Israeli wakuletee ng'ombe jike mwekundu asiye na doa, mkamilifu, ambaye hajatiwa nira bado;

na iwe, mji ulio karibu na yule aliyeuawa, wale wazee wake mji huo watwae mtamba katika kundi la ng'ombe, ambaye hajafanya kazi, wala hajakokota jembe la nira;

wazee wa mji huo na wamshushe yule mtamba mpaka bonde lenye maji ya mtoni, lisilolimwa wala kupandwa, wakamvunje yule mtamba shingo yake humo bondeni;