kutoka Shihori, hicho kijito kilichokabili Misri, hata mpaka wa Ekroni upande wa kaskazini, nchi inayohesabiwa kuwa ni ya hao Wakanaani; watawala watano wa hao Wafilisti; Wagaza, na Waashdodi, na Waashkeloni, na Wagiti, na Waekroni; tena Waavi,
1 Samueli 6:16 - Swahili Revised Union Version Na hao wakuu watano wa Wafilisti, hapo walipoyaona hayo, walirejea Ekroni siku iyo hiyo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wale wakuu watano wa Wafilisti walipoona hayo, walirudi Ekroni, siku hiyohiyo. Biblia Habari Njema - BHND Wale wakuu watano wa Wafilisti walipoona hayo, walirudi Ekroni, siku hiyohiyo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wale wakuu watano wa Wafilisti walipoona hayo, walirudi Ekroni, siku hiyohiyo. Neno: Bibilia Takatifu Wale watawala watano wa Wafilisti waliona haya yote, nao wakarudi Ekroni siku ile ile. Neno: Maandiko Matakatifu Wale watawala watano wa Wafilisti waliona haya yote, nao wakarudi siku ile ile mpaka Ekroni. BIBLIA KISWAHILI Na hao wakuu watano wa Wafilisti, hapo walipoyaona hayo, walirejea Ekroni siku hiyo hiyo. |
kutoka Shihori, hicho kijito kilichokabili Misri, hata mpaka wa Ekroni upande wa kaskazini, nchi inayohesabiwa kuwa ni ya hao Wakanaani; watawala watano wa hao Wafilisti; Wagaza, na Waashdodi, na Waashkeloni, na Wagiti, na Waekroni; tena Waavi,
Nao wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, Mbembeleze, upate kujua asili ya nguvu zake nyingi, na jinsi tutakavyoweza kumshinda, tupate kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu fedha elfu na mia moja.
aliwaacha wakuu watano wa Wafilisti, na Wakanaani wote, na Wasidoni, na Wahivi waliokaa katika kilima cha Lebanoni, toka mlima wa Baal-hermoni mpaka kuingia Hamathi.
Basi, wakalipeleka sanduku la Mungu mpaka Ekroni. Ikawa, sanduku la Mungu lilipofika Ekroni, watu wa Ekroni walipiga kelele, wakasema, Wamelileta hilo sanduku la Mungu wa Israeli kwetu, ili kutuua sisi na watu wetu.
Na hao ng'ombe wakashika njia moja kwa moja kwenda Beth-shemeshi; wakaiandama njia ya barabara, wakaenda wakilia, lakini hawakugeukia upande wa kulia wala wa kushoto; na wakuu wa Wafilisti wakawafuata hata kuufikia mpaka wa Beth-shemeshi.
Ndipo wakauliza, Na hayo matoleo ya kosa tutakayompelekea, yatakuwa ya namna gani? Na yawe majipu ya dhahabu matano, na panya wa dhahabu watano, sawasawa na idadi ya wakuu wa Wafilisti; kwa kuwa tauni moja ilikuwa juu yenu nyote, na juu ya wakuu wenu.