Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Naye akamwitikia, Mimi hapa.
1 Samueli 4:15 - Swahili Revised Union Version Basi Eli umri wake umepata miaka tisini na minane; na macho yake yamepofuka hata asiweze kuona. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakati huo, Eli alikuwa na umri wa miaka tisini na nane na macho yake yalikuwa yamepofuka. Biblia Habari Njema - BHND Wakati huo, Eli alikuwa na umri wa miaka tisini na nane na macho yake yalikuwa yamepofuka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakati huo, Eli alikuwa na umri wa miaka tisini na nane na macho yake yalikuwa yamepofuka. Neno: Bibilia Takatifu wakati huu Eli alikuwa na umri wa miaka tisini na nane, nayo macho yake yalikuwa yamepofuka hadi hakuweza kuona. Neno: Maandiko Matakatifu wakati huu Eli alikuwa na miaka tisini na minane nayo macho yake yalikuwa yamepofuka na hakuweza kuona. BIBLIA KISWAHILI Basi Eli umri wake umepata miaka tisini na minane; na macho yake yamepofuka hata asiweze kuona. |
Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Naye akamwitikia, Mimi hapa.
Akafanya hivi mkewe Yeroboamu, akaondoka, akaenda Shilo, akaja nyumbani kwa Ahiya. Basi Ahiya hakuweza kuona; kwa kuwa macho yake yamepofuka kwa sababu ya uzee wake.
Miaka ya maisha yetu ni sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Tena kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana wakati unapita upesi nasi kutokomea punde.
Ikawa wakati huo, Eli alipokuwa amelala mahali pake (tena macho yake yalikuwa yameanza kupofuka, hata asiweze kuona),
Naye Eli aliposikia kelele za kile kilio, akasema, Maana yake nini kelele za kishindo hiki? Yule mtu akafanya haraka, akaenda, akamwambia Eli.