Watumishi wake wote wakapita karibu naye; na Wakerethi wote, na Wapelethi wote, na Wagiti wote, watu mia sita walioandamana naye kutoka Gathi, wakapita mbele ya mfalme.
1 Samueli 30:9 - Swahili Revised Union Version Basi Daudi akaenda, yeye na wale watu mia sita waliokuwa pamoja naye, nao wakakifikia kijito Besori, ambapo wale walioachwa nyuma walikaa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa hiyo, Daudi akaondoka pamoja na wale watu 600 aliokuwa nao. Walipofika kwenye kijito cha Besori, wakawakuta baadhi ya watu waliotekwa wameachwa hapo. Biblia Habari Njema - BHND Kwa hiyo, Daudi akaondoka pamoja na wale watu 600 aliokuwa nao. Walipofika kwenye kijito cha Besori, wakawakuta baadhi ya watu waliotekwa wameachwa hapo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa hiyo, Daudi akaondoka pamoja na wale watu 600 aliokuwa nao. Walipofika kwenye kijito cha Besori, wakawakuta baadhi ya watu waliotekwa wameachwa hapo. Neno: Bibilia Takatifu Daudi pamoja na watu wake mia sita wakafika kwenye Bonde la Besori, ambapo wengine waliachwa nyuma, Neno: Maandiko Matakatifu Daudi pamoja na watu wake 600 wakafika kwenye Bonde la Besori, mahali ambapo wengine waliachwa nyuma, BIBLIA KISWAHILI Basi Daudi akaenda, yeye na wale watu mia sita waliokuwa pamoja naye, nao wakakifikia kijito Besori, ambapo wale walioachwa nyuma walikaa. |
Watumishi wake wote wakapita karibu naye; na Wakerethi wote, na Wapelethi wote, na Wagiti wote, watu mia sita walioandamana naye kutoka Gathi, wakapita mbele ya mfalme.
Daudi naye akawapandisha watu wake waliokuwa pamoja naye, kila mtu na watu wa nyumbani mwake; wakakaa katika miji ya Hebroni.
Basi Daudi akaondoka, yeye na hao watu mia sita aliokuwa nao, akamvukia Akishi, mwana wa Maoki, mfalme wa Gathi.
Lakini Daudi akaendelea kuwafuatilia, yeye na watu mia nne; kwa maana watu mia mbili walikaa nyuma, ambao walitaka kuzimia hata hawakuweza kukivuka hicho kijito Besori.