Hao wana wa Mkeni, huyo shemeji yake Musa, wakakwea juu kutoka katika huo mji wa mitende, pamoja na wana wa Yuda, na kuingia hiyo nyika ya Yuda, iliyo upande wa kusini wa Aradi; nao wakaenda na kukaa pamoja na watu hao.
1 Samueli 30:29 - Swahili Revised Union Version na kwa hao wa Rakali, na kwa hao wa miji ya Wayerameeli, na kwa hao wa miji ya Wakeni; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema wakazi wa Rakali, wakazi wa miji ya Wayerameeli, wakazi wa miji ya Wakeni, Biblia Habari Njema - BHND wakazi wa Rakali, wakazi wa miji ya Wayerameeli, wakazi wa miji ya Wakeni, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza wakazi wa Rakali, wakazi wa miji ya Wayerameeli, wakazi wa miji ya Wakeni, Neno: Bibilia Takatifu na Rakali; kwa wale waliokuwa katika miji ya Wayerameeli na ya Wakeni; Neno: Maandiko Matakatifu na Rakali; kwa wale waliokuwa katika miji ya Wayerameeli na ya Wakeni; BIBLIA KISWAHILI na kwa hao wa Rakali, na kwa hao wa miji ya Wayerameeli, na kwa hao wa miji ya Wakeni; |
Hao wana wa Mkeni, huyo shemeji yake Musa, wakakwea juu kutoka katika huo mji wa mitende, pamoja na wana wa Yuda, na kuingia hiyo nyika ya Yuda, iliyo upande wa kusini wa Aradi; nao wakaenda na kukaa pamoja na watu hao.
Sauli akawaambia Wakeni, Haya! Nendeni zenu, mkashuke ili kujitenga na Waamaleki, nisije nikawaangamiza ninyi pamoja nao; maana mliwatendea wana wa Israeli mema, walipopanda kutoka Misri. Basi hao Wakeni wakaondoka, wakajitenga na Waamaleki.
Ndipo wale Wazifi wakakwea kwa Sauli huko Gibea, wakasema, Je! Yule Daudi hakujificha kwetu ngomeni mwa Horeshi, kilimani pa Hakila upande wa kusini wa Yeshimoni?
Naye Akishi alipomwuliza, Je! Mmeshambulia upande gani leo? Na Daudi akasema, Juu ya Negebu ya Yuda, au, juu ya Negebu ya Wayerameeli, au, juu ya Negebu ya Wakeni.