Nikasema, Utafika mpaka hapa, lakini hutapita, Na hapa mawimbi yako yenye nguvu yatazuiliwa?
1 Samueli 30:2 - Swahili Revised Union Version nao wamewachukua mateka wanawake waliokuwamo wakubwa kwa wadogo; hawakuwaua wowote, ila wakawachukua, wakaenda zao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Walikuwa wameteka wanawake na watu wote waliokuwa mjini humo, wakubwa kwa wadogo. Hao waliowateka, waliondoka nao wakiwa hai, bila ya kumwua mtu yeyote. Biblia Habari Njema - BHND Walikuwa wameteka wanawake na watu wote waliokuwa mjini humo, wakubwa kwa wadogo. Hao waliowateka, waliondoka nao wakiwa hai, bila ya kumwua mtu yeyote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Walikuwa wameteka wanawake na watu wote waliokuwa mjini humo, wakubwa kwa wadogo. Hao waliowateka, waliondoka nao wakiwa hai, bila ya kumwua mtu yeyote. Neno: Bibilia Takatifu nao wakawa wamewachukua mateka wanawake pamoja na wote waliokuwamo humo, vijana na wazee. Hawakumuua yeyote, bali waliwachukua wakaenda zao. Neno: Maandiko Matakatifu nao wakawa wamewachukua mateka wanawake pamoja na wote waliokuwamo humo, vijana na wazee. Hawakuua yeyote, bali waliwachukua wakaenda zao. BIBLIA KISWAHILI nao wamewachukua mateka wanawake waliokuwamo wakubwa kwa wadogo; hawakuwaua wowote, ila wakawachukua, wakaenda zao. |
Nikasema, Utafika mpaka hapa, lakini hutapita, Na hapa mawimbi yako yenye nguvu yatazuiliwa?
Tena Daudi hakumhifadhi hai mume wala mke, ili kuwaleta Gathi maana alisema, Wasituchongee kusema, Ndivyo alivyofanya Daudi, tena ndivyo ilivyokuwa desturi yake wakati wote alipokaa katika nchi ya Wafilisti.
Wala hawakupotewa na kitu, mdogo wala mkubwa, wana wala binti, nyara wala chochote walichojitwalia hao; Daudi akavirudisha vyote.
Basi Daudi na watu wake walipoufikia mji, tazama, ulikuwa umechomwa moto; na wake zao, na watoto wao, wanaume kwa wanawake, wamechukuliwa mateka.