1 Samueli 30:10 - Swahili Revised Union Version Lakini Daudi akaendelea kuwafuatilia, yeye na watu mia nne; kwa maana watu mia mbili walikaa nyuma, ambao walitaka kuzimia hata hawakuweza kukivuka hicho kijito Besori. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini Daudi aliendelea kulifuatilia lile genge akiwa na watu 400, watu 200 wakabaki hapo kwani walichoka mno, wasiweze kuvuka kijito hicho. Biblia Habari Njema - BHND Lakini Daudi aliendelea kulifuatilia lile genge akiwa na watu 400, watu 200 wakabaki hapo kwani walichoka mno, wasiweze kuvuka kijito hicho. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini Daudi aliendelea kulifuatilia lile genge akiwa na watu 400, watu 200 wakabaki hapo kwani walichoka mno, wasiweze kuvuka kijito hicho. Neno: Bibilia Takatifu kwa kuwa watu mia mbili walikuwa wamechoka sana kuweza kuvuka hilo bonde. Lakini Daudi pamoja na watu mia nne wakaendelea kufuatia. Neno: Maandiko Matakatifu kwa kuwa watu 200 walikuwa wamechoka sana kuweza kuvuka hilo bonde. Lakini Daudi pamoja na watu 400 wakaendelea kufuatia. BIBLIA KISWAHILI Lakini Daudi akaendelea kuwafuatilia, yeye na watu mia nne; kwa maana watu mia mbili walikaa nyuma, ambao walitaka kuzimia hata hawakuweza kukivuka hicho kijito Besori. |
Naye Sauli na watu wote waliokuwapo pamoja naye wakakusanyika, wakaenda vitani; na tazama, huko upanga wa kila mtu ulikuwa juu ya mwenziwe, kukawa fujo tele kabisa.
Nao wakawapiga watu miongoni mwa Wafilisti siku ile kutoka Mikmashi mpaka Ayaloni; na hao watu walikuwa wamepungukiwa sana na nguvu.
Nao wakamkuta Mmisri nyikani wakamleta kwa Daudi, na kumpa chakula, naye akala; nao wakampa maji ya kunywa;
Kisha Daudi aliwafikia wale watu mia mbili, waliokuwa wametaka kuzimia, hata wasiweze kumfuata Daudi, wale waliowaacha wakae karibu na kijito cha Besori; nao wakatoka nje ili kumlaki Daudi, na kuwalaki hao watu waliokuwa pamoja naye, naye Daudi alipowakaribia hao watu, aliwasalimu.
Basi Daudi akaenda, yeye na wale watu mia sita waliokuwa pamoja naye, nao wakakifikia kijito Besori, ambapo wale walioachwa nyuma walikaa.