naye Malaika aliyeniokoa na maovu yote, na awabariki vijana hawa; jina langu na litajwe juu yao, na jina la baba zangu, Abrahamu na Isaka; na wawe wingi wa watu kati ya nchi.
1 Samueli 26:24 - Swahili Revised Union Version Tena, angalia, kama vile maisha yako yalivyokuwa na thamani machoni pangu, kadhalika na maisha yangu na yawe na thamani machoni pa BWANA, akaniokoe katika shida zote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tazama kama vile leo maisha yako yalivyokuwa na thamani mbele yangu, ndivyo na maisha yangu yawe na thamani mbele ya Mwenyezi-Mungu; naye akaniokoe kutoka kwenye taabu zote.” Biblia Habari Njema - BHND Tazama kama vile leo maisha yako yalivyokuwa na thamani mbele yangu, ndivyo na maisha yangu yawe na thamani mbele ya Mwenyezi-Mungu; naye akaniokoe kutoka kwenye taabu zote.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tazama kama vile leo maisha yako yalivyokuwa na thamani mbele yangu, ndivyo na maisha yangu yawe na thamani mbele ya Mwenyezi-Mungu; naye akaniokoe kutoka kwenye taabu zote.” Neno: Bibilia Takatifu Kwa hakika kama vile maisha yako yalivyokuwa ya thamani kwangu leo, vivyo hivyo maisha yangu na yawe na thamani kwa Mwenyezi Mungu na kuniokoa kutoka taabu zote.” Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hakika kama vile maisha yako yalivyokuwa ya thamani kwangu leo, vivyo hivyo maisha yangu na yawe na thamani kwa bwana na kuniokoa kutoka taabu zote.” BIBLIA KISWAHILI Tena, angalia, kama vile maisha yako yalivyokuwa na thamani machoni pangu, kadhalika na maisha yangu na yawe na thamani machoni pa BWANA, akaniokoe katika shida zote. |
naye Malaika aliyeniokoa na maovu yote, na awabariki vijana hawa; jina langu na litajwe juu yao, na jina la baba zangu, Abrahamu na Isaka; na wawe wingi wa watu kati ya nchi.
Naye Daudi akawajibu Rekabu na Baana, nduguye, wana wa Rimoni, Mbeerothi, akawaambia, Aishivyo BWANA, aliyenihifadhi roho yangu katika shida zote,
Mwamba wangu na ngome yangu, Nguzo yangu na mwokozi wangu Ngao yangu ninayemkimbilia, Huwatiisha watu wangu chini yangu.
Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili; Kwa mkamilifu utajionesha kuwa mkamilifu;
Huniponya na adui zangu; Naam, waniinua juu yao walioniinukia, Na kuniponya na mtu mjeuri.
Kwa kuwa limeniokoa na kila taabu; Na jicho langu limeridhika Kwa kuwatazama adui zangu.
Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.
wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwahimiza wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi.
Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-kondoo.
Wakati huo wakuu wa Wafilisti wakatokeza; kisha ikawa, kila mara walipotokeza, Daudi alipata ushindi zaidi kuliko watumishi wote wa Sauli hivyo jina lake likawa na sifa kuu.
Ikawa, Daudi alipokwisha kumwambia Sauli maneno hayo Sauli alisema, Hii ndiyo sauti yako, Daudi, mwanangu? Naye Sauli akapaza sauti yake, akalia.