Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

1 Samueli 24:5 - Swahili Revised Union Version

Lakini baadaye, moyo wake Daudi ukamchoma, kwa sababu amekata upindo wa vazi lake Sauli.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Daudi akaanza kufadhaika moyoni kwa sababu alikata pindo la vazi la Shauli kwa siri.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Daudi akaanza kufadhaika moyoni kwa sababu alikata pindo la vazi la Shauli kwa siri.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Daudi akaanza kufadhaika moyoni kwa sababu alikata pindo la vazi la Shauli kwa siri.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Baada ya hilo, dhamiri ya Daudi ikataabika kwa kukata upindo wa joho la Sauli.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Baada ya hilo, dhamiri ya Daudi ikataabika kwa kukata upindo wa joho la Sauli.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Lakini baadaye, moyo wake Daudi ukamchoma, kwa sababu amekata upindo wa vazi lake Sauli.

Tazama sura
Tafsiri zingine

1 Samueli 24:5
6 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa nini umelidharau neno la BWANA, na kufanya yaliyo mabaya machoni pake? Umempiga Uria, Mhiti, kwa upanga, nawe umemtwaa mkewe awe mke wako, nawe umemwua huyo kwa upanga wa Waamoni.

Ndipo moyo wake Daudi ukamchoma baada ya kuwahesabu hao watu. Naye Daudi akamwambia BWANA, Nimekosa sana kwa haya niliyoyafanya; lakini sasa, Ee BWANA, nakusihi uuondolee mbali uovu wa mtumishi wako; kwani nimefanya upumbavu kabisa.

kwa kuwa moyo wako ulikuwa mwororo, nawe ukajinyenyekeza mbele za BWANA, hapo ulipoyasikia maneno niliyoyanena juu ya mahali hapa, na juu ya wenyeji wake, ya kwamba watakuwa ukiwa na laana, nawe ulizirarua nguo zako, ukalia mbele zangu; basi, mimi nami nimekusikia wewe, asema BWANA.

Usiwaue, watu wangu wasije wakasahau; Uwatawanye kwa uweza wako, Na kuwaangamiza, Ee Bwana, ngao yetu.

Ndipo Abishai akamwambia Daudi, Mungu amemtia adui yako mikononi mwako leo; basi, niache nimpige kwa hilo fumo hadi chini kwa pigo moja, sitampiga mara ya pili.