Tena mtu wako, ambaye sitamtenga na madhabahu yangu, atakuwa mtu wa kukupofusha macho, na kukuhuzunisha moyo; tena wazao wote wa nyumba yako watakufa watakapokuwa watu wazima.
1 Samueli 22:21 - Swahili Revised Union Version Naye Abiathari akamweleza Daudi ya kwamba Sauli amewaua makuhani wa BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Abiathari alimweleza Daudi kuwa Shauli amewaua makuhani wa Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Abiathari alimweleza Daudi kuwa Shauli amewaua makuhani wa Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Abiathari alimweleza Daudi kuwa Shauli amewaua makuhani wa Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Abiathari akamwambia Daudi kuwa Sauli amewaua makuhani wa Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Akamwambia Daudi kuwa Sauli amewaua makuhani wa bwana. BIBLIA KISWAHILI Naye Abiathari akamweleza Daudi ya kwamba Sauli amewaua makuhani wa BWANA. |
Tena mtu wako, ambaye sitamtenga na madhabahu yangu, atakuwa mtu wa kukupofusha macho, na kukuhuzunisha moyo; tena wazao wote wa nyumba yako watakufa watakapokuwa watu wazima.
Na katika wana wa Ahimeleki, mwana wa Ahitubu, akaokoka mtu mmoja tu, aliyeitwa Abiathari, akamkimbilia Daudi.
Daudi akamwambia Abiathari, Siku ile alipokuwako Doegi, Mwedomi, nilijua hakika ya kuwa atamwambia Sauli; mimi nimewapatia watu wote wa jamaa ya baba yako kifo.