Kisha mfalme akamweka Benaya, mwana wa Yehoyada, mahali pake juu ya jeshi; na Sadoki, kuhani, mfalme akamweka mahali pa Abiathari.
1 Samueli 2:31 - Swahili Revised Union Version Angalia, siku zinakuja, nitakapoukata mkono wako, na mkono wa watu wa ukoo wa baba yako, hata nyumbani mwako hapatakuwako mzee. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Angalia siku zaja ambapo nitawaua vijana wote wa kiume katika jamaa yako na katika ukoo wako, hata hakutakuwa na mwanamume yeyote atakayeishi awe mzee. Biblia Habari Njema - BHND Angalia siku zaja ambapo nitawaua vijana wote wa kiume katika jamaa yako na katika ukoo wako, hata hakutakuwa na mwanamume yeyote atakayeishi awe mzee. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Angalia siku zaja ambapo nitawaua vijana wote wa kiume katika jamaa yako na katika ukoo wako, hata hakutakuwa na mwanamume yeyote atakayeishi awe mzee. Neno: Bibilia Takatifu Wakati unakuja nitakapozipunguza nguvu zenu na nguvu ya nyumba ya baba yenu, ili pasiwepo mtu katika jamaa yenu atakayeishi kuuona uzee, Neno: Maandiko Matakatifu Wakati unakuja nitakapozipunguza nguvu zenu na nguvu ya nyumba ya baba yenu, ili pasiwepo mtu katika mbari yenu atakayeishi kuuona uzee BIBLIA KISWAHILI Angalia, siku zinakuja, nitakapoukata mkono wako, na mkono wa watu wa ukoo wa baba yako, hata nyumbani mwako hapatakuwako mzee. |
Kisha mfalme akamweka Benaya, mwana wa Yehoyada, mahali pake juu ya jeshi; na Sadoki, kuhani, mfalme akamweka mahali pa Abiathari.
Lakini Walawi waliofarakana nami, wakapotea na kuvifuata vinyago vyao, hapo Waisraeli walipopotea, watachukua uovu wao wenyewe.
pamoja na Ahiya, mwana wa Ahitubu nduguye Ikabodi, mwana wa Finehasi, mwana wa Eli, kuhani wa BWANA huko Shilo, aliyevaa naivera. Tena hao watu hawakujua ya kwamba Yonathani ameondoka.
Siku hiyo nitayatimiza maneno yale yote niliyoyasema juu ya Eli kuhusu nyumba yake, tangu mwanzo hadi mwisho.
Nao Wafilisti wakajipanga juu ya Israeli; na walipopigana, Waisraeli wakapigwa na Wafilisti; waliowaua karibu elfu nne katika uwanja wa vita.