1 Samueli 12:8 - Swahili Revised Union Version Yakobo alipokuwa ameingia Misri, na baba zenu walipomlilia BWANA, ndipo BWANA akawapeleka Musa na Haruni, nao wakawatoa baba zenu kutoka Misri, wakawakalisha mahali hapa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Yakobo na jamaa yake walipokwenda Misri, na Wamisri walipowakandamiza, babu zenu walimlilia Mwenyezi-Mungu; naye akawatuma Mose na Aroni ambao waliwatoa babu zenu nchini Misri na kuwafanya mkae katika nchi hii. Biblia Habari Njema - BHND “Yakobo na jamaa yake walipokwenda Misri, na Wamisri walipowakandamiza, babu zenu walimlilia Mwenyezi-Mungu; naye akawatuma Mose na Aroni ambao waliwatoa babu zenu nchini Misri na kuwafanya mkae katika nchi hii. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Yakobo na jamaa yake walipokwenda Misri, na Wamisri walipowakandamiza, babu zenu walimlilia Mwenyezi-Mungu; naye akawatuma Mose na Aroni ambao waliwatoa babu zenu nchini Misri na kuwafanya mkae katika nchi hii. Neno: Bibilia Takatifu “Baada ya Yakobo kuingia Misri, walimlilia Mwenyezi Mungu awasaidie, naye Mwenyezi Mungu akawatuma Musa na Haruni, ambao waliwatoa baba zenu kutoka Misri na kuwakalisha mahali hapa. Neno: Maandiko Matakatifu “Baada ya Yakobo kuingia Misri, walimlilia bwana kwa ajili ya msaada, naye bwana akawatuma Musa na Haruni, ambao waliwatoa baba zenu kutoka Misri na kuwakalisha mahali hapa. BIBLIA KISWAHILI Yakobo alipokuwa ameingia Misri, na baba zenu walipomlilia BWANA, ndipo BWANA akawapeleka Musa na Haruni, nao wakawatoa baba zenu kutoka Misri, wakawakalisha mahali hapa. |
Ilikuwa siku ile ile moja, BWANA akawatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri kwa majeshi yao.
Hawa ni Haruni yeye yule, na Musa yeye yule, BWANA aliowaambia, akisema, Watoeni wana wa Israeli watoke nchi ya Misri sawasawa na majeshi yao.
jinsi baba zetu walivyoteremkia Misri, nasi tulikaa Misri muda mrefu, nao Wamisri walitutenda vibaya sana, na baba zetu pia;
Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.
Basi BWANA aliwapa Israeli nchi hiyo yote, ambayo aliapa kwamba atawapa baba zao; nao wakaimiliki, na kukaa humo.
akawaambia wana wa Israeli, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Niliwatoa Waisraeli kutoka Misri, nami niliwaokoa ninyi kutoka kwa mikono ya Wamisri, na ya falme zote zilizowaonea;
Samweli akawaambia watu, Ni yeye BWANA aliyewaweka Musa na Haruni, yeye ndiye aliyewatoa baba zenu kutoka nchi ya Misri.