Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama damu, zitakuwa kama sufu.
1 Samueli 12:7 - Swahili Revised Union Version Basi sasa simameni, ili niwahutubie mbele za BWANA, kwa kutaja matendo yote ya haki ya BWANA, aliyowatendea ninyi na baba zenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sasa simameni papo hapo mlipo ili mimi na nyinyi tuhukumiwe mbele ya Mwenyezi-Mungu, nami nitawahutubia kuhusu matendo yake ya ajabu ambayo aliyatenda ili kuwaokoa nyinyi na babu zenu. Biblia Habari Njema - BHND Sasa simameni papo hapo mlipo ili mimi na nyinyi tuhukumiwe mbele ya Mwenyezi-Mungu, nami nitawahutubia kuhusu matendo yake ya ajabu ambayo aliyatenda ili kuwaokoa nyinyi na babu zenu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sasa simameni papo hapo mlipo ili mimi na nyinyi tuhukumiwe mbele ya Mwenyezi-Mungu, nami nitawahutubia kuhusu matendo yake ya ajabu ambayo aliyatenda ili kuwaokoa nyinyi na babu zenu. Neno: Bibilia Takatifu Sasa basi, simameni hapa, kwa sababu nitakabiliana nanyi kwa ushahidi mbele za Mwenyezi Mungu wa matendo yote ya haki yaliyofanywa na Mwenyezi Mungu kwenu na kwa baba zenu. Neno: Maandiko Matakatifu Sasa basi, simameni hapa, kwa sababu nitakabiliana nanyi kwa ushahidi mbele za bwana wa matendo yote ya haki yaliyofanywa na bwana kwenu na kwa baba zenu. BIBLIA KISWAHILI Basi sasa simameni, ili niwahutubie mbele za BWANA, kwa kutaja matendo yote ya haki ya BWANA, aliyowatendea ninyi na baba zenu. |
Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama damu, zitakuwa kama sufu.
nami nitawaingiza katika jangwa la mataifa, na huko ndiko nitakakoteta nanyi uso kwa uso.
akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewaambia ninyi habari zake ndiye Kristo.
Mbali na kelele za hao wapigao mishale, katika mahali pa kuteka maji, Hapo watatangaza matendo ya haki ya BWANA; Naam, matendo ya haki ya kutawala kwake katika Israeli. Ndipo watu wa BWANA waliposhuka malangoni.