Nao watanijua kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wao, niliyewatoa katika nchi ya Misri, nipate kukaa kati yao; ni mimi BWANA Mungu wao.
1 Samueli 10:18 - Swahili Revised Union Version akawaambia wana wa Israeli, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Niliwatoa Waisraeli kutoka Misri, nami niliwaokoa ninyi kutoka kwa mikono ya Wamisri, na ya falme zote zilizowaonea; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Walipowasili aliwaambia, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Niliwatoa Waisraeli nchini Misri, nikawaokoa nyinyi kutoka kwa Wamisri na falme nyingine zilizowakandamiza. Biblia Habari Njema - BHND Walipowasili aliwaambia, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Niliwatoa Waisraeli nchini Misri, nikawaokoa nyinyi kutoka kwa Wamisri na falme nyingine zilizowakandamiza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Walipowasili aliwaambia, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Niliwatoa Waisraeli nchini Misri, nikawaokoa nyinyi kutoka kwa Wamisri na falme nyingine zilizowakandamiza. Neno: Bibilia Takatifu naye akawaambia, “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: ‘Niliwatoa Israeli kutoka Misri, nami niliwaokoa toka nguvu za Misri na falme zote zilizowadhulumu.’ Neno: Maandiko Matakatifu naye akawaambia, “Hili ndilo asemalo bwana, Mungu wa Israeli: ‘Niliwatoa Israeli kutoka Misri, nami niliwaokoa toka nguvu za Misri na falme zote zilizowaonea.’ BIBLIA KISWAHILI akawaambia wana wa Israeli, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Niliwatoa Waisraeli kutoka Misri, nami niliwaokoa ninyi kutoka katika mikono ya Wamisri, na ya falme zote zilizowaonea; |
Nao watanijua kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wao, niliyewatoa katika nchi ya Misri, nipate kukaa kati yao; ni mimi BWANA Mungu wao.
Tena hapo mtakapokwenda kupiga vita katika nchi yenu, kupigana na adui awaoneaye ninyi, ndipo mtakapopiga sauti ya kugutusha kwa tarumbeta; nanyi mtakumbukwa mbele za BWANA, Mungu wenu, nanyi mtaokolewa na adui zenu.
Kisha malaika wa BWANA alikwea kutoka Gilgali kwenda Bokimu. Akasema, Mimi nimewaleta ninyi mkwee kutoka nchi ya Misri, nami nimewaleta hadi nchi niliyowaapia baba zenu; nami nilisema, Mimi milele sitalivunja hilo agano langu nililoagana nanyi;
Yakobo alipokuwa ameingia Misri, na baba zenu walipomlilia BWANA, ndipo BWANA akawapeleka Musa na Haruni, nao wakawatoa baba zenu kutoka Misri, wakawakalisha mahali hapa.