Ndipo wakuu wakamwendea Yeremia, wakamwuliza; naye akawaambia sawasawa na maneno aliyoamriwa na mfalme. Basi wakaacha kunena naye; maana neno lile halikujulikana.
1 Samueli 10:15 - Swahili Revised Union Version Babaye mdogo Sauli akasema, Tafadhali niambie, huyo Samweli aliwaambiaje? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yule baba mdogo wa Shauli akamwambia, “Tafadhali, niambie kile alichokuambia Samueli.” Biblia Habari Njema - BHND Yule baba mdogo wa Shauli akamwambia, “Tafadhali, niambie kile alichokuambia Samueli.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yule baba mdogo wa Shauli akamwambia, “Tafadhali, niambie kile alichokuambia Samueli.” Neno: Bibilia Takatifu Babaye mdogo Sauli akasema, “Niambie Samweli amekuambia nini.” Neno: Maandiko Matakatifu Babaye mdogo Sauli akasema, “Niambie Samweli amekuambia nini.” BIBLIA KISWAHILI Babaye mdogo Sauli akasema, Tafadhali niambie, huyo Samweli aliwaambiaje? |
Ndipo wakuu wakamwendea Yeremia, wakamwuliza; naye akawaambia sawasawa na maneno aliyoamriwa na mfalme. Basi wakaacha kunena naye; maana neno lile halikujulikana.
Basi babaye mdogo akamwuliza Sauli na mtumishi wake, Je! Mlikwenda wapi? Naye akajibu, Tulikwenda ili kuwatafuta hao punda; na tulipoona ya kwamba hawakuonekana, tulimwendea Samweli.
Lakini Sauli akamjibu babaye mdogo, Alituambia waziwazi ya kuwa hao punda wamekwisha onekana. Lakini habari ya ufalme, ambayo Samweli alimwambia, hakuitaja.