1 Samueli 10:12 - Swahili Revised Union Version Naye akajibu mtu mmoja wa mahali hapo, akasema, Na baba yao ni nani? Kwa hiyo ikawa mithali, Je! Sauli pia yumo miongoni mwa manabii? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu fulani, mkazi wa mahali hapo, akasema, “Je, baba yao ni nani?” Hivyo kukazuka methali isemayo, “Je, hata Shauli ni mmoja wa manabii?” Biblia Habari Njema - BHND Mtu fulani, mkazi wa mahali hapo, akasema, “Je, baba yao ni nani?” Hivyo kukazuka methali isemayo, “Je, hata Shauli ni mmoja wa manabii?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu fulani, mkazi wa mahali hapo, akasema, “Je, baba yao ni nani?” Hivyo kukazuka methali isemayo, “Je, hata Shauli ni mmoja wa manabii?” Neno: Bibilia Takatifu Mtu mmoja ambaye aliishi huko akajibu, “Je, naye baba yao ni nani?” Basi ikawa mithali, kusema, “Je, Sauli pia yumo miongoni mwa manabii?” Neno: Maandiko Matakatifu Mtu mmoja ambaye aliishi huko akajibu, “Je, naye baba yao ni nani?” Basi ikawa mithali, kusema, “Je, Sauli pia yumo miongoni mwa manabii?” BIBLIA KISWAHILI Naye akajibu mtu mmoja wa mahali hapo, akasema, Na baba yao ni nani? Kwa hiyo ikawa mithali, Je! Sauli pia yumo miongoni mwa manabii? |
Imeandikwa katika manabii, Na wote watakuwa wamefundishwa na Mungu. Basi kila aliyesikia na kujifunza kwa Baba huja kwangu.
Basi Yesu akawajibu, akasema, Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenituma.
Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.
Basi akaenda Nayothi huko Rama, na Roho ya Mungu ikamjia yeye naye, akaendelea mbele, huku anatabiri, mpaka kufika Nayothi huko Rama.
Naye akavua nguo zake, akatabiri mbele ya Samweli, akalala uchi mchana kutwa na usiku kucha siku ile. Kwa hiyo watu wakasema, Je! Sauli pia yumo miongoni mwa manabii?