Mimi ni ndugu yenu Yoane. Kwa njia ya kuungana na Yesu, ninashirikiana nanyi katika mateso, katika ufalme wake na katika kuvumilia. Mimi nilikuwa nimepelekwa katika kisanga kinachoitwa Patimo, kwa sababu nilihubiri Neno la Mungu na ukweli ulioshuhudiwa na Yesu.