Nehemia 7:5 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
5 Mungu akanipa moyo kuwakusanya viongozi na watu kwa kujua ukoo zao. Nikapata kitabu cha ukoo za watu waliorudi toka katika uhamisho mara ya kwanza, na hawa ndio waliokuwa wameandikwa ndani yake.
Nikamwomba Mungu nikisema: “Ee Mungu, kumbuka mambo yote Tobia na Sanibalati waliyotenda, hata yule Noadia, nabii mwanamuke, na manabii wengine waliotaka kuniogopesha.”
Hao walitafuta kitabu cha vizazi vyao kati ya wengine walioandikwa katika kitabu cha ukumbusho za ukoo, lakini ukoo wao haukuonekana. Kwa hiyo hawakuruhusiwa kutiwa katika kazi ya ukuhani maana walihesabiwa kuwa wachafu.
Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa sawa hivi ninavyokuwa, na neema yake niliyopewa haikukuwa ya bure, lakini nilitumika zaidi sana kuliko mitume wote wengine. Hakika si mimi, lakini ni neema ya Mungu inayokuwa pamoja nami.