Basi, watu wakaanza kazi katika mwezi wa pili wa mwaka wa pili nyuma ya kufikia kwenye nyumba ya Mungu katika Yerusalema. Zerubabeli, mwana wa Saltieli, Yesua mwana wa Yosadaki, wandugu zao wengine, makuhani, Walawi na watu wengine wote waliorudi Yerusalema kutoka katika uhamisho, wakajiunga nao katika kazi hiyo. Walawi wote waliokuwa na umri wa miaka makumi mbili au zaidi, walichaguliwa kwa kusimamia kazi ya kuijenga upya nyumba ya Yawe.