Nehemia 6:18 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
18 Wengi kati ya Wayuda walishirikiana naye kutokana na kiapo chao maana alikuwa mukwe wa Sekania mwana wa Ara. Zaidi ya yote, Yehohanani mwana wake, alikuwa amemwoa binti Mesulamu mwana wa Berekia.
Sehemu inayofuata ikiwa ni sehemu yao ya pili ikajengwa upya na Hanania mwana wa Selemia, akishirikiana na Hanuni mwana wa sita wa Zalafi. Mesulamu mwana wa Berekia, akajenga upya sehemu inayoelekeana na chumba chake.
Sehemu inayofuata ikajengwa upya na Meremoti mwana wa Uria, mujukuu wa Hakosi. Sehemu inayofuata ikajengwa upya na Mesulamu mwana wa Berekia, mujukuu wa Mesezabeli. Sehemu inayofuata ikajengwa upya na Zadoki mwana wa Bana.