Nehemia 12:47 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 200247 Watu wote wa Israeli, tangu wakati wa Zerubabeli na Nehemia, walitoa matoleo ya kila siku kwa ajili ya waimbaji na walinzi wa milango. Zaidi ya yote, watu wa Israeli wakatoa matoleo kwa ajili ya Walawi, nao Walawi wakatenga sehemu kwa ajili ya wazao wa Haruni. 參見章節 |
Haya ndiyo majina ya makuhani na Walawi waliorudi toka katika uhamisho pamoja na Zerubabeli mwana wa Saltieli, na Kuhani Mukubwa Yesua. Makuhani walikuwa: Seraya, Yeremia, Ezra, Amaria, Maluku, Hatusi, Sekania, Rehumu, Meremoti, Ido, Ginetoni, Abiya, Miyamini, Madia, Bilga, Semaya, Yoyaribu, Yedaya, Salu, Amoki, Hilkia na Yedaya. Hao walikuwa ni wakubwa wa makuhani na wandugu zao wakati wa Yesua.
Yoyakimu alipokuwa Kuhani Mukubwa, makuhani hawa walikuwa wakubwa wa ukoo zao: ukoo wa Seraya: Meraya; ukoo wa Yeremia: Hanania; ukoo wa Ezra: Mehulamu; ukoo wa Amaria: Yehohanani; ukoo wa Maluku: Yonatani; ukoo wa Sebania: Yosefu; ukoo wa Harimu: Adina; ukoo wa Meraioti: Helkayi; ukoo wa Ido: Zakaria; ukoo wa Ginetoni: Mesulamu; ukoo wa Abiya: Zikiri; ukoo wa Miniamini: ukoo wa Moadia: Piltai; ukoo wa Bilga: Samua; ukoo wa Semaya: Yehonatani; ukoo wa Yoaribu: Matenayi; ukoo wa Yedaya: Uzi; ukoo wa Salayi: Kalayi; ukoo wa Amoki: Eberi; ukoo wa Hilkia: Hesabia; ukoo wa Yedaya: Netaneli.