Nehemia 12:43 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
43 Siku hiyo, watu wakatoa sadaka nyingi na kufurahi maana Mungu aliwafanya kuwa na furaha kubwa. Vilevile wanawake na watoto, wote wakafurahi. Vigelegele vya furaha toka katika Yerusalema vikasikilika mbali.
Siku iliyofuata ambayo ilikuwa siku ya makumi mbili na tatu ya mwezi wa saba, Solomono akawaaga watu waende kwao, wakishangilia na kufurahi ndani ya moyo kwa sababu ya mazuri ambayo Yawe alimutendea Daudi, Solomono na kwa watu wake Waisraeli.
Kisha wakati wa kuzindua ukuta wa Yerusalema Walawi wakatafutwa kila pahali walipokaa kwa kuja Yerusalema kusherehekea kwa furaha pamoja na shukrani na nyimbo, wakitumia matoazi, vinubi na zeze.
na kuwapa wale wanaoomboleza katika Sayuni taji la maua pahali pa majivu juu ya kichwa, mafuta ya kuangarisha kwa furaha pahali pa maombolezo, nguo ya sifa pahali pa moyo muzito. Nao wataitwa miti ya mialo ya haki, Yawe aliyopanda kuonyesha utukufu wake.
Halafu wabinti zao watafurahi na kucheza, vijana na wazee watashangilia kwa furaha. Nitageuza maombolezo yao kuwa furaha, nitawafariji na kuwapa furaha pahali pa huzuni.
sauti za arusi na za furaha, sauti za waimbaji wakati wanaleta sadaka za shukrani katika nyumba ya Yawe. Wataimba hivi: Mumushukuru Yawe wa majeshi kwa sababu Yawe ni muzuri, kwa maana wema wake unadumu milele. Nitairudishia inchi hii hali yake ya zamani. –Ni Yawe anayesema.
Vilevile katika siku zenu za furaha, kama vile sikukuu za mwandamo wa mwezi na sikukuu nyingine, mutapiga baragumu hizi wakati munapotoa sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za amani. Hapo mimi Mungu wenu nitawakumbuka. Mimi ni Yawe, Mungu wenu.
Lakini wakubwa wa makuhani na walimu wa Sheria wakachukizwa kwa kuona miujiza aliyoifanya na watoto waliokuwa wakilalamika katika hekalu, wakisema: “Usifiwe wewe, mwana wa Daudi!”
Nalo kundi la watu waliomutangulia Yesu na lile la watu waliofuata nyuma yake, wakaanza kulalamika, wakisema: “Usifiwe wewe Mwana wa Daudi! Abarikiwe huyu anayekuja kwa jina la Bwana! Mungu asifiwe juu mbinguni!”