Kwa vile ambavyo hesabu ya makuhani ilikuwa ndogo, hawakuweza kuchuna nyama wale wote. Kwa hiyo, wandugu zao Walawi wakawasaidia mpaka walipomaliza kazi hiyo. Wakati ule, makuhani wengine zaidi walikuwa wamekwisha kujitakasa. (Walawi walijiweka katika hali ya usafi zaidi kuliko makuhani.)