Watu waliposikia Sheria, wakaguswa ndani ya mioyo yao, halafu wote wakaanza kulia. Hivyo Nehemia aliyekuwa mutawala na Ezra kuhani na mwandishi, pamoja na Walawi waliofundisha watu wakawaambia watu wote: “Siku hii ni siku takatifu kwa Yawe, Mungu wenu, hivyo musiomboleze wala kulia.