kwa ajili ya mikate mitakatifu, sadaka za unga za kawaida, sadaka za kuteketezwa kwa moto za kawaida, sadaka za siku za Sabato, sikukuu za mwandamo wa mwezi, sikukuu nyingine zilizowekwa, vitu vingine vitakatifu, sadaka za kusamehewa zambi, kwa kuwafanyia upatanisho watu wa Israeli na kazi nyingine zozote za nyumba ya Mungu wetu.