Lakini Waisraeli hawakukuwa waaminifu juu ya vile vitu vilivyotolewa viangamizwe maana Akana mwana wa Karmi, mujukuu wa Zabedi, wa ukoo wa Zera, wa kabila la Yuda, alitwaa vimoja kati ya vitu vilivyoamriwa viteketezwe. Kwa hiyo hasira ya Yawe ikawaka juu ya Waisraeli.